Mauzo na manunuzi ya hisa DSE yapanda.

Licha ya Tanzania kuwa kwenye mchakato wa Uchaguzi Mkuu, Thamani ya jumla ya miamala ya uwekezaji kwa hisa na hatifungani katika soko la hisa la Dar es Salaam imeongezeka zaidi na kufikia Shilingi Bilioni 33.73 kutoka Shilingi Bilioni 1.99, hii ikielezwa kuwa ni imani waliyonayo wawekezaji kwa serikali, kwa mujibu wa ripoti ya mwenendo wa biashara kwenye soko hilo.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko hilo Bw. Moremi Marwa amewaambia waandishi wa habari kuwa kiwango hicho kinatokana na kuongezeka kwa ukwasi na uwekezaji katika segmenti ya hisa kutoka Shilingi Bilioni 0.64 hadi Shilingi Bilioni 0.78 wakati kwa upande wa hatifungani uwekezaji umeongezeka kutoka Shilingi Bilioni 1.35 hadi Bilioni 32.95.

Kuhusu mchanganuo wa wawekezaji, Bw.Moremi Marwa amesema wawekezaji wa ndani walichangia asilimia 43 katika mauzo na asilimia 36 katika manunuzi ya uwekezaji wote sokoni kwa upande wa hisa, huku wawekezaji wa nje wakichangia asilimia 64 katika manunuzi na asilimia 57 katika mauzo yote sokoni.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Dkt. Magufuli aendelea kuinadi ilani akirejea Dodoma.

Read Next

Mashindano ya magari kufanyika Arusha mwezi ujao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!