Mkataba wa kupiga marufuku silaha za nyuklia.

FILE PHOTO: A serviceman walks past anti-aircraft defence mobile missile systems during the Keys to the Sky competition at the International Army Games 2017 at the Ashuluk shooting range outside Astrakhan, Russia August 5, 2017. REUTERS/Maxim Shemetov/File Photo – RC116195B0A0

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa nchi 50 zimeidhinisha mkataba wa Umoja wa Mataifa wa kupiga marufuku silaha za nyuklia na kuchochea kutekelezwa kwake katika muda wa siku 90.

Hatua hiyo imesifiwa na wanaharakati wa kupambana na matumizi ya nyuklia lakini inapingwa vikali na Marekani na mataifa mengine yenye ushawishi mkubwa wa nyuklia.

Hadi kufikia Ijumaa ya wiki iliyopita mkataba huo ulikuwa na saini kutoka mataifa 49 na maafisa wa Umoja wa Mataifa wamesema Honduras imekuwa nchi ya 50 kuridhia mkataba huo.

Beatrice Fihn, Mkurugenzi mtendaji wa kampeni ya kimataifa ya kukomesha silaha za nyuklia, amesema hatua hiyo imechukua muda wa miaka 75 tangu shambulizi la kutisha la nyuklia dhidi ya miji ya Hiroshima na Nagasaki na kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa ambao ulitoa kipaumbele kuzuia silaha za nyuklia.

Marekani imeyaandikia mataifa yaliyotia saini mkataba huo na kusema serikali yake inaamini kuwa yalifanya ”kosa la kimkakati” na kuyahimiza kubatilisha misimamo yao.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Watoto watoa Ujumbe wa amani kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Read Next

Dkt. Magufuli aendelea kuinadi ilani akirejea Dodoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!