Shirika la Madini la Twiga laonyesha uwezo mkubwa.

Kampuni ya Madini ya Barrick imesema Shirika la Madini la Twiga limeonyesha uwezo mkubwa wa kutengeneza thamani ya ushirika ikiwa ni mwaka mmoja pekee tangu kuanzishwa kwake.

Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick Bwana Mark Bristow ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kufuatia ziara yake ya robo mwaka mgodini.

Amesisitiza kwamba thamani kubwa imeonekana ndani ya mfupi jambo ambalo linaashiria nguvu kubwa ya ushirika wa kwanza na wa aina yake barani Afrika.

Shirika la Twiga ni ubia kati ya Kampuni ya Madini ya Barrick na Serikali ya Tanzania, ambapo shirika hilo linasimamia menejimenti ya rasilimali za Barrick nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na kutekeleza makubaliano ya mgawanyo wa kiuchumi baina ya pande hizo mbili.

Shirika la Madini TWIGA lilianzishwa wakati Kampuni ya Barrick inayoendesha shughuli za uchimbaji madini katika migodi ya Buzwagi, Bulyanhulu na North Mara ilipochukua shughuli za iliyokuwa Acacia Mining Septemba mwaka jana na kuingia makubaliano na Serikali ya Tanzania.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Mashindano ya magari kufanyika Arusha mwezi ujao.

Read Next

Rais Dkt. Magufuli apiga kura Kijiji cha Chamwino Ikulu Mkoani Dodoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!