Watoto watoa Ujumbe wa amani kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Watoto wamewaasa wazazi na walezi kote nchini kuendelea kudumisha amani katika kipindi chote cha uchaguzi mkuu kwa kutokubali kushangilia matokeo yoyote yatakayotangazawa na mamlaka tofauti na Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC sambamba na kutoshiriki maandamano yoyote haramu.

Watoto wametoa ujumbe huo wakati wakiongoza ibada maalum kwa ajili ya kuombe Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotaraji kufanyika katikati ya Juma lijalo Oktoba 28 iliyofanyika katika kanisa la T.A.G Mnadani Revival Temple.

Ujumbe huo umeeleza kuwa endapo wazazi watashawishika na kushiriki katika maandamano yoyote haramu yanaweza kusababisha vurugu zitakazowasababishia ulemavu na vifo hivyo kuwaacha Watoto wakiwa yatima jambo litakalowaathiri.

Mchungaji kiongozi wa Kanisa hilo anaendelea kuwakumbusha Watanzania thamani ya amani ambayo Taifa limejaaliwa tangu Uhuru na kwamba jamii inaowajibu wa kuendelea kuilinda ikiwa ni Pamoja na kuchagua viongozi watakaoidumisha.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Serikali ya CCM yapanga kununua meli tano kubwa za uvuvi.

Read Next

Mkataba wa kupiga marufuku silaha za nyuklia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!