Taasisi iliyopata kibali cha kuangalia mwenendo wa uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 nchini ‘The Right Way’ imeeleza kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ulikuwa Uhuru na haki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya ‘The Right Way’ ambayo ilipewa kibali cha kutoa elimu kwa mpiga kura pamoja kufuatilia mwenendo wa uchaguzi mkuu amesema uchaguzi huo umezingatia vigezo vyote vya uchaguzi na kubainisha kwamba umekuwa wa Uhuru na haki.
Aidha imeipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC kwa kufanikisha hatua hiyo huku akiwasihi Watanzania kuendelea na maisha kama kawaida kwa kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi.
Taasisi ya The Right Way imesema taarifa hiyo kuhusu uchaguzi mkuu ni ya awali hivyo taarifa kamili ya taasisi hiyo itatolewa rasmi baada ya mwezi mmoja.