Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi linamshikilia mtuhumiwa mmoja anaejulikana kwa jina la Sistor katabi akiwa na vipande viwili vya meno ya tembo eneo la Ilalangulu kata ya Kibaoni tarafa ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoani Katavi.
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi ASP Benjamin Kuzaga amesema kuwa jeshi la polisi linamshikilia Sistor Katabi akiwa na vipande viwili vya meno ya Tembo.
“Amekamatwa akiwa na vipande viwili vya meno Tembo, mkia wa Tembo, vipande viwili vikavu vya ini la Tembo, kipande cha ngozi la sikio la Tembo, kipande cha kucha cha mguu wa Tembo, kipande cha pua cha Nyati, kipande cha ngozi ya nyoka, vipande kumi na mbili vya nondo” alisema Kamanda huyo wa Polisi.
Pia amewataka wananchi wanaojihusisha na vitendo vya ujangili kuacha shughuli hizo.