Kamati ya Mashindano ya Miss Utalii Tanzania kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwemo Bendi ya Malaika, wamezindua tamasha la kutangaza utalii wa fukwe zilizopo katika jijiji la Dar es Salaam ikiwa ni mkakati wa kuzifanya fukwe hizo kuvutia watalii wengi zaidi lakini pia kuchangia mapato ya Serikali.
Rais wa Mashindano hayo Gideon Chipungahelo amewaambia waandishi wa habari kuwa mpango huo unaanza na ufukwe wa Hoteli ya Dynasty uliopo eneo la Kunduchi Ununio jijini Dar es Salaam ambako kumeandaliwa Tamasha la Full Moon Party kesho jioni.
Naye Mkurugenzi Mtemdaji wa Hoteli ya Dynasty Beach Resort Manase Mwakale amesema wameamua kuandaa tamasha hilo ambalo asili yake ni nchini Thailand ambako kumekuwa na mafanikio makubwa katika kuvutia utalii, hali ambayo inawezekana pia kwa Tanzania.