Biashara na uwekezaji Nchini vyaendelea kuwa imara.

Takwimu za kibiashara zimeonyesha kuwa shughuli za uchumi na uwekezaji hapa nchini zimeendelea kuimarika licha ya uwepo wa mchakato wa uchaguzi mkuu ambao unafikia kilele chake wiki hii.

Miongoni mwa viashiria vya uchumi kuwa imara ilikuwa ni miamala ya Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) katika wiki iliyoishia Tarehe 30 Oktoba 2020, ambapo kwa mujibu wa Afisa Mtendaji Mkuu wa DSE Moremi Marwa, upekee wa mfumo wa soko hilo unaruhusu shughuli za ununuzi na uuzaji wa hisa kufanyika bila kuathiriwa na shughuli za kisiasa.

Akitoa hesabu ya ukubwa wa soko la ndani katika wiki iliyoishia Oktoba 30, Afisa Mtendaji Mkuu huyo amesema limeongezeka kwa kiwango cha Shilingi Bilioni 42.77 ikilinganishwa na wiki iliyoishia Oktoba 23 ambapo mtaji ulikuwa ni Shilingi Trilioni 9.06 hadi Trilioni 9.11.

Kwa upande wa thamani ya miamala ya Hati Fungani ya Shilingi Bilioni 26.44, wawekezaji ambao ni taasisi na kampuni ilikuwa Shilingi bilioni 21.55 sawa na asilimia 81, huku miamala ya wawekezaji wa rejareja ikiwa ni Shilingi Biloni 4.9 sawa na asilimia 19.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Jeshi la Polisi (M) Dodoma laonya.

Read Next

Wananchi wa Dsm wapuuza maandamano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!