Jeshi la Polisi (M) Dodoma laonya.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limeonya kuwa halitoruhusu shughuli za wananchi kusimamishwa na baadhi ya watu wanaotaka kufanya maandamano ya kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28 kwani maandamano hayo hayakubaliki kisheria.

Mapema majira ya Asubuhi vikosi vya Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma vimefanya mazoezi ya utayari wa mwili vikiongozwa na kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma SACP Gilles Muroto kwa kuzunguka maeneo mbalimbali ya jiji.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma SACP Gilles Muroto anabainisha kuwa Pamoja na kufanya mazoezi ya utayari vikosi vipo tayari kukabiliana na mtu au kikundi kitakachojaribu kufanya maandamano.

Pia akabainisha namna Jeshi la Polisi mkoani hapa lilivyojipanga kuimarisha ulinzi na usalama kuelekea sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambazo kwa mara ya kwanza zitafanyika jijini Dodoma.

Channel Ten imezunguka katika viunga mbalimbali vya jiji la Dodoma na kukuta hali ikiwa shwari huku wananchi wakiendelea na shughuli zao ambapo baadhi wakaeleza ushiriki wao katika kudumisha amani ya nchi.

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Taasisi ya ‘The Right Way’ yasema uchaguzi ulikuwa huru na haki.

Read Next

Biashara na uwekezaji Nchini vyaendelea kuwa imara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!