Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wameendelea na Shughuli zao za kujitafutia kipato kama Kawaida wakipuuza wito wa baadhi ya viongozi wa Vyama vya Upinzani wa kuhamasisha Maandamano wakilalamikia walichodai mchakato wa uchaguzi mkuu kufuatia matokeo yaliyoonyeshwa kushindwa katika uchaguzi huo uliofanyika Octoba 28.
Channel Ten ilitembelea Maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam yakiwemo Maeneo ya Manzese,Tandale, Kinondoni Magomeni na Kariakoo na kujionea watu mbalimbali yakiwemo makundi ya vijana wakiendelea na shughuli zao za kujitafutia kipato.
Aidha katika Eneo la Kariakoo hali imekuwa ya Utulivu huku wafanyabiashara ndogondogo wakiendelea na Shughuli zao kama kawaida.
Wakati hali ya jiji la dsm ikiendelea kuwa Shwari Kiongozi Mkuu wa Umoja wa Wanaharakati Wazalendo -Uwasti ametawaka Watanzania Kufanya kazi kwa Kumuunga Mkono Rais Mteule Mhe Dkt. John Pombe Magufuli na Kupuuza Wito wa Maandamano ambayo hayana tija kwa Taifa.