Kituo cha Kimataifa cha Mabasi Mbezi Luis kuanza majaribio tahere 25 mwezi huu.

Ujenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Mabasi Mbezi Luisi kilichopo Mbezi Jijini DSM kinatarajia kuanza Majaribio ya kutumika kwa Mabasi ya Mikoani tarehe 25 mwezi huu, baada ya Ujenzi wake kukamilika kwa asilimia 90.

Mkurugenzi wa Jjiji la DSM Siporah Liana akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi, amesema Kazi hiyo inaendelea Usiku na Mchana ili ikamilike mwishoni mwa mwezi huu, ambapo ametoa wito kwa wafanyabiashara kujitokeza kuanzia Jumatatu Novemba 9 kkwa njia ya mtandao, ili kuomba nafasi za kufanyia biashara.

Amesema kwa upande wa wafanyabiashara wadogo maarufu machinga, mama na baba lishe wao hawatahusika na mchakato wa kuomba kwa njia ya Mtandao kwa kuwa wao wamewekewa utaratibu maalum kwa ajili ya kuendesha biashara katika eneo hilo.

Aidha Mkurugenzi huyo wa Jiji amesema pamoja na ujenzi huo kufikia asilimia 90, wamefanikia kuokoa kiasi cha Billion 13 na kwamba hadi utakapokamilika ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara ya kuingia na kutoka katika Kituo hicho, watakuwa wameokoa fedha nyingi kutoka kiasi cha Shilingi Bilioni 50.9 ambayo ilikuwa gharama ya Mkataba wa Ujenzi wa Kituo hicho.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Kongamano la Amani, Viongozi wa Dini mbalimbali washiriki.

Read Next

Rais Dkt. Mwinyi afanya uteuzi wa Makamu wa Pili wa Rais.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!