Kongamano la Amani, Viongozi wa Dini mbalimbali washiriki.

Viongozi mbalimbali wa kidini nchini wameshiriki kongamano la Shukrani la kumalizika kwa uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28 mwaka huu kwa salama na amani.

Akizungumza katika kongamano hilo Askofu Mkuu wa Mtandao wa kimataifa wa Makanisa ya WAPO MISSION INTERNATIONAL Sylvester Gamanywa, amesema kuwa Uchaguzi wa kuwapata viongozi wa nchi umetoa funzo kubwa kwa mataifa mengine kutokana na kufanyika katika mazingira ya amani na utulivu, huku akieleza kuwa vyama vilivyoshiriki uchaguzi ni muda wao kuunga juhudi za kimaendeleo baada ya kumalizika kwa uchaguzi.

Kwa upande wake Mufti wa Zanzibar Sheikh Saleh Al Kaabi amesema panapokuwa na amani ndipo panapokuwa na maendeleo hivyo ametumia wasaa huo kueleza kuwa Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi kazi yao Sasa ni kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo zaidi.

Naye Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship Zacharia Kakobe akizungumzia kongamano hilo lenye kauli mbiu iliyobeba ujumbe wa “Amani yetu, Maendeleo yetu” inaonyesha kuwa kila mtanzania anapaswa kuunga juhudi za serikali na kufanya kazi za kimaendeleo akiungwa mkono na Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Rais Dkt. Magufuli kuzindua Bunge la 12 Jumanne ijayo.

Read Next

Kituo cha Kimataifa cha Mabasi Mbezi Luis kuanza majaribio tahere 25 mwezi huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!