Rais Dkt. Magufuli kuzindua Bunge la 12 Jumanne ijayo.

Mkutano wa kwanza wa Bunge la Kumi na Mbili umepangwa kufanyika Jumanne ya wiki ijayo jijini Dodoma, na hivyo wabunge wote wateule wakitakiwa kuripoti katika ofisi za bunge Dodoma, kuanzia leo hadi Jumatatu.

Akitoa taarifa mbele ya waandishi wa Habari jijini Dodoma, Katibu wa Bunge Bw. STEVEN KAGAIGAI amewataka wabunge wote wateule waje na nyaraka zifuatazo, Hati ya kuchaguliwa kuwa mbunge na zingine kama nakala ya kitambulisho cha Taifa, Cheti cha kuzaliwa pamoja na cheti cha ndoa.

Bunge hilo la kumi na mbili katika mkutano wake wa kwanza, litazinduliwa na kuhutubiwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, na linatarajiwa kuahirishwa tarehe Kumi ya mwezi huu.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Katibu wa Rais wa Zanzibar aapishwa.

Read Next

Kongamano la Amani, Viongozi wa Dini mbalimbali washiriki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!