Bunge lamuidhinisha Majaliwa kuwa Waziri Mkuu.

Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, limemuidhinisha mbunge wa Ruangwa Mhe. Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kumpa asilimia 100 ya kura zote za ndiyo.

Mara baada ya kutolewa kwa matokeo hayo, Mhe. Spika akampa nafasi Waziri Mkuu Mteule, kuongea na wabunge.

Pamoja na mambo mengine, lakini Mhe. Majaliwa akawaahidi waheshimiwa wabunge juu ya utendaji wa baraza lijalo la mawaziri.

Aidha, bunge hilo lilimchagua Dkt. Tulia Akson kuwa Naibu Spika baada ya kupata kura 350 za ndiyo na kura nne za hapana, ambapo kabla ya kupigwa kura alipewa nafasi ya kuomba kura.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Rais Dkt. Mwinyi afanya uteuzi wa Makamu wa Pili wa Rais.

Read Next

Uwezekano wa kutokea Janga la Wakimbizi TIGRAY.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!