Uwezekano wa kutokea Janga la Wakimbizi TIGRAY.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia wakimbizi UNHCR limesema lina wasiwasi kwamba kutatokea janga la wakimbizi iwapo raia wataendelea kukimbia mapigano katika mkoa wa Tigray kaskazini mwa Ethiopia.

Wanajeshi wa serikali wamekuwa wakipambana na wapiganaji wa mkoa huo kwa muda sasa ambapo nchi ya Sudan mpaka sasa imepokea zaidi ya wakimbizi 10,000 wa Ethiopia tangu mapigano hayo yaanze na mashirika ya misaada yanasema hali ya Tigray inazidi kuwa mbaya.

Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesema jeshi la nchi hiyo limepata miili ya wanajeshi wengine ikiwa imefungwa kamba na kupigwa risasi huko Tigray.

Wakati hayo yakijri Ethiopia imewakamata maafisa 17 wa jeshi kwa kosa la uhaini, ikiwashutumu kwa kula njama na mamlaka za mkoa wa Tigray, ambako serikali inaendesha operesheni ya kijeshi.

Waziri Mkuu Abiy Ahmed alituma jeshi katika Mkoa wa Tigray wiki iliyopita baada ya mzozo wa miezi kadhaa na chama cha TPLF kinachotawala mkoani humo ambapo waziri huyo mkuu amenukuliwa akisema chama hicho kilivuka mstari mwekundu kwa kushambulia kambi mbili za jeshi, madai ambayo hata hivyo chama hicho cha TPLF kimekanusha.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Bunge lamuidhinisha Majaliwa kuwa Waziri Mkuu.

Read Next

Walibya wakubaliana kufanya Uchaguzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!