Walibya wakubaliana kufanya Uchaguzi.

Umoja wa Mataifa unasema Walibya wamekubaliana kufanya uchaguzi katika kipindi cha miezi kumi na nane ijayo wakati ambapo juhudi za kidiplomasia zinaendelea ili kusitisha mapigano yaliyoizonga nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika kwa kipindi cha karibu mwongo mmoja sasa.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa Stephanie Williams amewaambia waandishi wa habari kuwa wawakilishi kutoka kote nchini humo wamebuni mpango wa kufikisha kikomo kipindi cha mpito na kuandaa uchaguzi wa urais na wabunge utakaokuwa wazi, utakaomjumuisha kila mmoja na wa kuaminika.

Kulingana na mpango huo, uchaguzi utafanyika katika kipindi kisichozidi miezi kumi na nane.

Mazungumzo hayo ya Tunisia yanalenga kubuni mpango na serikali ya mpito itakayofanya maandilizi ya uchaguzi huo pamoja na kutoa huduma katika nchi iliyokabiliwa na uharibifu mkubwa kutokana na mzozo ikiwemo vita vya wenye kwa wenyewe vilivyodumu kwa muda mrefu.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Uwezekano wa kutokea Janga la Wakimbizi TIGRAY.

Read Next

Rais Magufuli azindua Bunge la 12 na Kuhutubia Taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!