Rais Magufuli azindua Bunge la 12 na Kuhutubia Taifa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli, amewaagiza viongozi wa serikali kuanzia ngazi za chini, kutenga siku ya kusikiliza kero za wananchi, badala ya kungoja ziara za viongozi wa kitaifa, ndio watatue kero hizo.

Mhe. Dkt. Magufuli amelitoa agizo hilo bungeni jijini Dodoma, wakati alipokuwa akizindua Bunge la kumi na mbili, ambalo kwa sasa linao wabunge 359.

Aidha, Mhe. Rais akaweka wazi nia ya serikali kushirikiana kikamilifu na sekta binafsi katika kukuza uchumi, na mantiki hiyo akaagiza kuhamishwa kituo cha uwekezaji nchini (TIC) kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kwenda Ofisi ya Rais, ili urasimu unaoendelea, udhibitiwe.

Pamoja na mambo mengine, Mhe. Dkt. Magufuli akawaaidi wamachinga, kuboreshwa kwa vitambulisho vyao, ili viweze kuwasaidia kupata mikopo benki, huku watumishi nchini, nao wakiahidiwa kuboreshewa maslahi yao.

Katika kuhakikisha sekta ya uvuvi inatoa mchango zaidi kwenye pato la taifa, Mhe. Rais Magufuli akaliambia taifa kupitia Bunge, mpango wa serikali kununua meli nane za uvuvi wa bahari kuu, pamoja na ujenzi wa bandari kubwa ya uvuvi itakayotoa ajira ya zaidi ya watu 30,000.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Walibya wakubaliana kufanya Uchaguzi.

Read Next

Rais Magufuli ahimiza uwajibikaji wa Viongozi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!