Mazungumzo ya Makubaliano ya Kuunda Serikali ya Mpito Nchini Libya.

Pande hasimu nchini Libya zimekamilisha mazunguzmo ya wiki moja yaliyofadhiliwa na Umoja wa Mataifa bila ya kufikia makubaliano ya kuunda serikali ya mpito ambayo ingeongoza nchi hiyo kuelekea uchaguzi mkuu wa Desemba mwaka unaokuja.

Kaimu mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Libya Stephanie Williams amewaambia waandishi habari mjini Tunis, kuwa mkutano huo uliowakutanisha wajumbe 75 wa Libya haukujadili majina ya watu watakaounda serikali lakini mazungumzo yaliyofanyika yanatia moyo.

Mazungumzo hayo yalifanyika chini ya shinikizo kali kutoka jumuiya ya kimataifa baada ya Umoja wa Mataifa kufanikiwa kupatikana mkataba wa kusitisha mapigano kati ya pande hasimu nchini Libya mwezi uliopita.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Rais Magufuli ahimiza uwajibikaji wa Viongozi.

Read Next

Serikali ya Ethiopia yadai kuukamata Mji wa Alamata.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!