Serikali ya Ethiopia yadai kuukamata Mji wa Alamata.

Serikali ya Ethiopia imesema leo kuwa imeukamata mji mwingine wa jimbo la kaskazini la Tigray baada ya karibu wiki mbili za mapigano katika mzozo unaotishia kuteteresha hali ya usalama kwenye eneo la pembe ya Afrika.

Kikosi kazi kilichoundwa na waziri mkuu Abey Ahmed kimesema vikosi vya serikali vimeukomboa mji wa Alamata kutoka mikononi mwa wapiganaji wa chama cha TPLF kinachoongoza mkoa wa Tigray.

Kadhalika wamedai kuwa wapiganaji wa TPLF wameukimbia mji huo wakiwa na wafungwa 10,000 huku wakaazi wengi wa eneo hilo pia wamekimbia wakihofia kusajiliwa kama wapiganaji wa TPLF.

Viongozi wa TPLF hawajatoa maelezo yoyote kuhusiana na madai ya kukamatwa kwa mji wa Alamata ulio karibu na mpaka wa jimbo lingine la Ethiopia la Amhara na kiasi kilometa 120 kutoka mji mkuu wa Tigray, Mekelle.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Mazungumzo ya Makubaliano ya Kuunda Serikali ya Mpito Nchini Libya.

Read Next

Waziri Mkuu Tanzania azindua uchepushaji wa maji ya Mto Rufiji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!