Rais Mwinyi afanya ziara yakushtukiza hospitali ya Rufaa ya Mnazi moja Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema haridhishwi na mazingira ya utendaji kazi wa Hopitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja na kutoa muda wa miezi mitatu kwa wafanyakazi wa hospitali hiyo kubadilika.

Mhe. Rais Dkt. Mwinyi Kauli hiyo ameitoa baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Hosptali hiyo iliyolenga kuangalia utendaji kazi ambapo amebaini kuwepo kwa changamoto nyingi zinazoikabili hospitali hiyo licha ya kutengewa fungu la fedha kwa ajili ya uendeshaji, ambapo katika kipindi cha Agosti na Septemba mwaka huu hospitali hiyo ilipokea shilingi Bilioni 3.1, lakini ameshuhudia upungufu wa vifaa.

Ziara ya rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi, imetokana na malalamiko ya wananchi kuwa hawaridhishwi na huduma zinazotolewa.

Akizungumzia kero alizokutana nazo katika hospitali hiyo amesema kwa kiasikikubwa zinatokana na utendaji usioridhisha hospitalini hapo.

Mapema asubuhi aliwatembelea wafanya biashara wa soko la Kijangwani amabo siku ya Jumatatu Mkuu wa mkoa mjini magharibi aliwapa siku tatu wafanya biashara hao kuondoka katika eneo hilo nakuhamia katika soko kwerekwe Ijtimai Wilaya ya Magharibi B.

Akielezea sababu zakuwaondoa wafanya kazi hao mkuu wa mkoa wa mjini Magharibi Hassan Khatibu Hassan amesema lengo nikupisha ujenzi wa soko lakisasa na kituo cha mabasi ya abiria.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Waziri Mkuu Tanzania azindua uchepushaji wa maji ya Mto Rufiji.

Read Next

Waziri Mkuu atoa siku 15 Hospitali ya Uhuru ikamilike.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!