Waziri Mkuu atoa siku 15 Hospitali ya Uhuru ikamilike.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ametoa siku 15 kwa uongozi ya Wilaya ya Chamwino, Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) na Suma JKT wahakikishe ujenzi wa hospitali ya Uhuru katika Halmashauri ya Chamwino unakamilika.

Akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa hospitali hiyo, Waziri Mkuu amesema lengo ni kuhakikisha hospitali hiyo inazinduliwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ifikapo Desemba 9, mwaka huu ili kutimiza maono yake ya ujenzi wa hospitali hiyo.


Waziri Mkuu ameonyesha kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi huo.


Aidha, Waziri Mkuu ameeleza kuwa anataka kuona vifaa vyote vya ujenzi wa hospitali hiyo vinatoka kwenye viwanda vya ndani ili kuharakisha ukamilishwaji wa hospitali hiyo hasa marumaru kwani tayari kuna viwanda vikubwa vinavyozalisha bidhaa hiyo kwa ubora wa hali ya juu.


Waziri Mkuu katika ziara hiyo alifuatana na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (TAMSEMI), Mhandisi Joseph Nyamhaga na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge.
#KilichoBoraKabisa

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Rais Mwinyi afanya ziara yakushtukiza hospitali ya Rufaa ya Mnazi moja Zanzibar.

Read Next

Wanaotuhumiwa kuwapa Mimba Wanafunzi Mwanza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!