Ujenzi wa Kivuko cha Mafia wafikia asilimia 98.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema mradi wa ujenzi wa kivuko kipya cha Mv. Kilindoni Hapa Kazi Tu kitakachokuwa kinafanya safari kati ya kisiwa cha Mafia na Nyamisati, umefikia asilimia 98 na kwamba ifikapo Desemba 15 mwaka huu kitaingia majini kwa mara ya kwanza.

Waziri Mkuu amebainisha hayo mara baada ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa kivuko hicho kinachojengwa katika eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam na kampuni ya M/S Songoro Marine Boat Yard ya Mwanza kwa gharama ya sh. Bilioni 5.3.

Waziri Mkuu pia ametumia fursa hiyo kuwapongeza watanzania walioajiriwa kwenye mradi huo kwa kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu jambo ambalo limezaa matunda katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Awali, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle alisema hadi sasa mkandarasi ameshakamilisha kazi zote kubwa ikiwemo ufungaji wa mfumo wa injini, usukani, mabomba ya maji, viti, milango, vyoo na upakaji wa rangi.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Wanaotuhumiwa kuwapa Mimba Wanafunzi Mwanza.

Read Next

Rais Magufuli akagua Ujenzi wa Ofisi za Ikulu Dodoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!