Rais Magufuli akagua Ujenzi wa Ofisi za Ikulu Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo amekagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Ikulu Mkoani Dodoma na kuonesha kuridhishwa na kiwango na kasi ya ujenzi wa majengo ya ofisi hizo unaofanywa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Ujenzi wa Ofisi hizo ulioanza Februari 17 mwaka huu, unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 3 ijayo na unafanywa kwa usanifu na muonekano sawa na Ofisi za Ikulu zilizopo Jijini Dar es Salaam, ambapo kwa mujibu wa Msimamizi wa ujenzi wa ofisi hizo, Luteni Kanali George William Nyisa, ujenzi huo utakamilika kwa wakati uliopangwa.

Mhe. Rais Magufuli ameelezea kufurahishwa kwake na uimara wa nguzo na kuta zilizotumika ambapo amesema ni fahari kubwa kwa Taifa kujenga ofisi yake ya Ikulu kwa kutumia Jeshi lake badala ya kutumia wakandarasi kutoka nje ya nchi.

Mhe. Rais Magufuli pia amezungumza na Vijana wa JKT wanaoshiriki ujenzi huo ambapo amekumbusha ahadi yake kuwa vijana hao 2,424 wataandikishwa JWTZ mara watakapomaliza jukumu la ujenzi wa Ofisi za Ikulu.

Pamoja na kuwapongeza vijana hao, Mhe. Rais Magufuli pia amewapongeza vijana wa kiraia wanaoshiriki katika ujenzi huo ambao ni mafundi, na amewaahidi kuwa atawaangalia mara baada ya kumaliza kazi hiyo.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Ujenzi wa Kivuko cha Mafia wafikia asilimia 98.

Read Next

TAKUKURU yatoa siku 14 kwa wakandarasi 16 wanaotekeleza miradi ya REA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!