TAKUKURU yatoa siku 14 kwa wakandarasi 16 wanaotekeleza miradi ya REA.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Mbungo ametoa kipindi cha siku 14 kwa wakandarasi wote wanaotekeleza miradi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kurejesha vifaa ghafi vyenye thamani ya shilingi bilioni 10 kwa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kama mikataba yao inavyoelekeza ya kwamba mkandarasi anapaswa kurejesha vifaa ghafi baada ya kukamilisha kazi.

Akikabidhi vifaa ghafi hivyo kwa TANESCO, Mkurugenzi Mkuu huyo wa TAKUKURU Brigedia Jeneral John Mbungo amesema kwa kuanzia tayari TAKUKURU imekabidhi vifaa ghafi kwa TANESCO vyenye thamani ya bilioni 1.2 ambavyo vilikuwa vikitumika na wakandarasi 16 waliokuwa wanatekeleza miradi ya REA awamu ya pili mkoani Iringa huku akisema jambo hilo ni takwa la kisheria na kuna kila sababu ya kulitekeleza.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Dkt. Tito Mwinuka amewakumbusha wakandarasi wanaotekeleza miradi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kutimiza wajibu wao kwa wakati muafak

Comments

comments

Anthony Shija

Read Previous

Rais Magufuli akagua Ujenzi wa Ofisi za Ikulu Dodoma.

Read Next

ATCL yazindua safari ya Kwanza Geita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!