ATCL yazindua safari ya Kwanza Geita.

Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limezindua safari yake ya kwanza kwenda Mkoani Geita, huku wananchi wakihamasishwa kutumia fursa hiyo kujiletea maendeleo ya kiuchumi.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho akizindua safari hiyo amesema uwepo wa safari za ndege kwenda Geita kunafungua fursa ya kukuza uchumi wa mkoa huo ambao ni mzalishaji wa mazao mengi, uvuvi, utajiri wa madini na utalii.

Amesema kuzinduliwa kwa usafiri huo kumedhihirisha nia ya dhati ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha mapinduzi hivyo amewataka wana Geita kutumia fursa hiyo kuongeza na kukaribisha uwekezaji kwa kuwa usafiri wa ndege ni wa uhakika na wa haraka zaidi.

Amesema hivi sasa serikali inaboresha viwanja vingine vya ndege katika mikoa ya Arusha, Iringa na Ruvuma ili kuiwezesha ATCL kuhudumia miji na mikoa 15 kutoka miji na mikoa 11 ya sasa.

Baadhi ya viongozi waliohudhuria uzinduzi huo akiwemo Mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel na Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Chato wakazungumzia namna wananchi wa Geita watakavyotumia fursa ya uwepo wa usafiri wa anga.

Awali MKurugenzi Mkuu wa ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi alieleza kuwa ndege hiyo itakuwa ikifanya safari zake mara mbili kwa wiki Jumamosi na Jumatatu na baada ya Januari 18 mwaka huu safari hizo zitaongezeka na kuwa tatu siku za Jumatatu, Alhamisi na Jumamosi kutokea DSM, GEITA na kurejea DSM kupitia Mwanza.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

TAKUKURU yatoa siku 14 kwa wakandarasi 16 wanaotekeleza miradi ya REA.

Read Next

Makamu wa Rais aongoza Kikao cha mawaziri Ikulu, Dodoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!